IQNA

Msomi wa Misri: Kutajwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa Katika Qur'ani Kunaakisi Utambulisho Wake wa Kiislamu

16:29 - April 16, 2025
Habari ID: 3480552
IQNA – Rais wa zamani wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar amesema kuwa Qur'ani Tukufu inaangazia utambulisho wa Kiislamu wa Msikiti wa Al-Aqsa.

Akizungumza katika mkutano wa kila wiki wa Msikiti wa Al-Azhar wiki hii, Sheikh Ibrahim al-Hudhud amesema kwamba Surah Al-Isra inaanza kwa kutaja Msikiti wa Al-Aqsa, jambo linaloonesha kuwa msikiti huu ni sehemu isiyotenganishwa na utambulisho wa Ummah wa Kiislamu.

Amesema kuwa jina la Msikiti wa Al-Aqsa katika Qur'an, kinyume na wanavyodhani baadhi ya watu, halipo tu katika Surah Al-Isra, bali pia linapatikana katika Surah nyingine kadhaa, zikiwemo Al-Baqarah, Al Imran, Al-Aaraf, Al-Qassas, Muminun na Qaaf.

Mji mtakatifu wa Al-Quds (Jerusalem) utakuwa mahali pa kukusanyika kwa watu Siku ya Kiyama, na ndipo viumbe watafufuliwa siku hiyo, alieleza al-Hudhud.

Aliongeza kuwa Mtume Mtukufu (SAW) alisisitiza fadhila za Msikiti wa Al-Aqsa na kuwaagiza Waislamu kwenda kwenye msikiti huo, na akasema: “Ikiwa mtu atawasha taa ndani yake, ni kama vile ameswali ndani yake.”

Mwanazuoni huyo pia alieleza kuwa Qur'anI haiuhusishi msikiti huu na Wayahudi. Salah Ashur alikuwa mwanazuoni mwingine aliyehutubia mkutano huo. Alikanusha juhudi za wavamizi wa Kizayuni za kuharibu Msikiti wa Al-Aqsa kwa kisingizio cha kutafuta Hekalu la Suleiman, na kusema kuwa juhudi hizo ni kisingizio cha kuufanya msikiti huo kuwa wa Kiyahudi na kuuvunjia heshima.

Aliongeza kuwa Al-Quds na Palestina zitabaki kuwa za Waarabu, bila kujali ni kwa muda gani uhasama utaendelea au ni kwa kiasi gani mkoloni adui atajaribu kupotosha historia.

3492706

Habari zinazohusiana
Kishikizo: azhar al aqsa
captcha