IQNA

Waislamu Uingereza wanyimwa ruhusa kufungua msikiti Windsor

21:58 - December 16, 2021
Habari ID: 3474683
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Waislamu Windsor wanatafakari kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Uingereza baada ya kunyimwa idhini ya kujenga msikiti katika mji wa Windsor.

Waislamu wamenunua jengo (kwenye picha) ambalo lingetumiwa na familia 30 kama eneo la ibada lakini ombi la kubadilisha jingo hilo limekataliwa.

Tayari Waislamu wamekuwa wakitumia jengo hilo katika Barabara y Maidenhead  kwa muda wa miaka 10 kama eneo la kufanya ibadaa na sherehe mbali mbali. Hatahivyo manispaa ya eneo hilo limepinga ombi la Waislamu kubadilisha jengo hilo kuwa msikiti.

Wakuu wa manispaa wanadai ujenzi wa msikiti utavuruga mandhari ya kijani kibichi na kutakuwa na msongamano wa magari katika Barabara ya Maidenhead. Waislaamu wamekanusha madai kuwa msikiti ungevuruga mandhari ya kijani kibichi na kwamba msongamano wa magari unaodaiwa ni wa lisaa limoja tu katika siku za Ijumaa.

3476945

captcha