Sehemu moja ya ujumbe huo wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei imeeleza: "ninatoa mkono wa pole na hongera kuaga dunia kwa namna ya kufa shahidi balozi mwanajihadi na mchapakazi wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Yemen Hasan Irlu, kwa familia yake azizi na kwa marafiki na wanafikra wenzake aliokuwa nao katika awamu mbalimbali za jihadi na juhudi zake za muda mrefu."
Katika ujumbe wake huo, Ayatullah Khamenei ameongezea kwa kusema: "faili lake ni la kujivunia kutokana na jihadi yake ya kisiasa, jitihada zake za kidiplomasia na harakati za kijamii. Kaka zake wawili wametangulia kabla yake kupata daraja ya kufa shahidi. Rehma za Mwenyezi Mungu zimshukie ndugu huyu mwanajihadi pamoja na familia yake yenye subira, basira na moyo wa kujitolea."
Shahidi Irlu
Hasan Irlu, balozi wa Iran nchini Yemen ambaye alikuwa majeruhi wa silaha za kemikali za wakati wa vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa Baath wa Iraq dhidi ya Iran, alipatwa na ugonjwa wa corona nchini Yemen alikopelekwa kikazi, lakini kwa masikitiko alirejea nchini akiwa mahututi kutokana na baadhi ya nchi kuchelewa kutoa ushirikiano.
Licha ya juhudi zilizofanywa za kumpatia huduma zote za matibabu zilizohitajika, siku ya Jumanne, mwanadiplomasia huyo wa Iran alifikia daraja tukufu ya kufa shahidi.