IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Algeria kufanyika kupitia intaneti

13:38 - January 13, 2022
Habari ID: 3474803
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Algeria yatafanyika kwa njia ya intaneti, imetangaza Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini nchini humo.

Taarifa ya wizara hiyo imesmea uamuzi huo umechukuliwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19 jambo ambalo limepelekea iwe vigumu kuandaa mashinano ya washiriki kukutana ana kwa ana.

Nara na kali mbiu ya mashindano yam waka huu ni  وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا (na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo) ambayo ni sehemu ya aya ya nne ya Surah Al-Muzzammil.

Mashidano hayo yamepengwa kufanyika Februari 17-19 2022 ambapomajaji watakuwa ni kutoka Algeria na nchi kadhaa za Kiislamu.

Washiriki katika Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Algeria wanapaswa kuwa chini ya umri wa miaka 25 na wasiwe walishika nafasi ya kwanza hadi ya tatu ya mashindano yaliyopita.

Algeria ni nchi iliyo kaskazini mwa Afrika na asilimia 99 ya wakazi wake ni Waislamu.

4028059

captcha