IQNA

Mtaalamu wa Algeria: Wakoloni walidhoofisha Qur'ani Afrika

18:16 - January 03, 2022
Habari ID: 3474758
Mtaalamu mmoja wa Qur'ani Tukufu nchini Algeria amesema kuwa wakoloni walitekeleza njama za makusudi za kudhoofisha nafasi na hadhi ya Qur'ani barani Afrika.

Msomi wa Qur'ani Algeria Sheikh Nureddin Aby Lahya aliyasema hayo alipohtubu katika warsha ya kujadili 'Hali ya Qiraa na Tajwid ya Qur'ani Tukufu Barani Afrika' ambayo ilifanyika mwezi Novemba  kwa njia ya intaneti.

Warsha hiyo iliandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO) kwa ushirkiano na  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) pamoja na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Algeria.

Akizungumza katika kikao hicho, Sheikh Abu Lahya amesema hivi sasa anatayarisha tafsiri mpya ya Qur'ani kwa kuzingatia matukio ya hivi sasa duniani.

Ameongeza kuwa, kwa karne nyingi Qur'ani Tukufu ilikuwa na hadhi ya juu kaskazini mwa Afrika na bara zima la Afrika kwa ujumla lakini wakati wa ukoloni kulitekelezwa njama za makusudi za kudhoofisha nafasi ya Qur'ani Tukufu katika jamii na njama hiyo ilishuhudiwa wazi kabisa nchini Algeria.

Amelalammika kuwa hivi sasa ingawa kuna Idhaa ya Qur'ani nchini Algeria lakini jitihada za serikali za kustawisha Qur'ani bado hazijafika kiwango kinachotakiwa.

Ameendelea kusema kuwa mafundisho ya Qur'ani nchini Algeria yako katika juzuu chache tuu na wanafunzi wengi wako katika mashinikizo kuacha masomo ya Qur'ani.

Colonialism Hit Quran Position in Africa: Experts

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa na Wahubiri wa Eneo la Sahara Sheikh Yusuf Mushriya naye pia amesema watu wa Afrika walianza kujenga vyuo vya Qur'ani katika karne za awali wakati Uislamu ulipoingia barnai humo.  Aidha amesema vyuo vya Qur'ani vilikuwa na nafasi muhimu sana katika kudumisha utambulisho wa Algeria na kukabiliana na ukoloni. Ameongeza kuwa wakati wa ukoloni waalimu wengi wa Qur'ani na wanafunzi wao waliohifadhi Qur'ani waliuawa wakiwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya wanajeshi wa utawala wa kikoloni.

Aidha amesema Wiki ya Qur'ani Algeria huandaliwa kila mwaka Algeria wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW na ni wakati huo ndio pia hufanyika mashindano ya Qur'ani. Amesema familia za Algeria zinalipa umuhimu mkubwa suala la watoto kujifunza Qur'ani.

4023232

captcha