IQNA

18:54 - January 26, 2022
Habari ID: 3474854
TEHRAN (IQNA)- Duru ijayo ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia itafanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Muongozo yatakuwa na wawakilishi wa nchi za Kiislamu na zisizo kuwa za Kiislamu.

Mashindano ya mwaka huu ambayo ni ya 42 yatakuwa na kategoria tano na washindi watapta zawadi za hadi Riyali za Kisaudi milioni 2.7 au Euro takribani laki sita.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu, Dawah na Muongozo Saudia Sheikh Abdullatif Al-Asheikh amesema mashindano hayo yanalenga kuwahimiza Waislamu kote duniani kujifunza na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na pia kujikurubisha zaidi na Kitabu hicho kitakatifu.

Amesema zawadi za fedha taslimu mwaka huu zitakuwa zaidi ya miaka iliyopita. Aidha amebaini kuwa kategoria mpya ya mwaka huu ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu sambamba na kuwa na uwezo wa kusoma kwa qiraat zote saba.

Aidha amesema tayari barua za mwaliko zimeshatumwa kwa nchi mbali mbali kwa lengo la kuarifisha washiriki.

3477553

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: