IQNA

Mchezaji wa Nigeria achanjia mradi wa msikiti Cameroon

15:07 - January 30, 2022
Habari ID: 3474867
TEHRAN (IQNA)- Ahmed Musa, Kapteni wa Timu ya Soka ya Nigeria ametoa mchango wa dola 1,500 kusaidia katika mradi wa upanuzi wa Msikiti wa Jamia wa Garoua kaskazini mwa Cameroon.

Wachezaji na maafisa wa timu hiyo ambayo ni maarufu kama Super Eagles wamekuwa wakiswali katika msikiti huo tokea wawasili katika mji huo.

Mchango huo ni kwa ajili ya kuunga mkono mradi wa upanuzi wa msikiti huo. Ukarimu huo wa Ahmed Musa ni moja kati ya michango ambaye hutoa kuwasaidia watu binafsi na taasisi.

Afisa wa timu hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwa amesema Musa aliweka nia ya kusaidia ukarabati wa msikiti huo  mwa ya kwanza aliposwali hapo.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mchezaji aliwahi kuichezea mara nyingi zaidi timu ya taifa ya Nigeria kwani hadi sasa amecheza Mechi 104 tokea mechi yake ya kwanza mwaka 2011.

4032317/

captcha