IQNA

19:40 - February 21, 2022
Habari ID: 3474956
TEHRAN (IQNA)- Duru ya mwisho ya mchujo katika mashindano ya Qur’ani Tukufu ya wasichana imeanza nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Jumatatu.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la  Zawadi ya Qur’ani Tukufu ya Hessa bin Muhammad yanatazamiwa kuendelea hadi Machi 10. Hii ni duru ya tisa ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Sultan bin Khalifa Al Nahyan kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu na Idara ya Wakfu UAE.

Jumla ya wasichana 130 wanashiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika kategoria 11.

4037872

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: