IQNA

Harakati za Qur'ani

Wasichana wa Algeria washiriki kozi za Qur'ani za majira ya joto

17:34 - August 08, 2024
Habari ID: 3479246
IQNA - Wizara ya Wakfu na masuala ya Kiislamu ya Algeria inasema wasichana wa nchi hiyo wamekuwa wakifurahia sana kozi za Qur'ani Tukufu za msimu huu wa majira ya joto nchini humo..

Wasichana wa rika tofauti wamechukua kozi hizo katika majimbo mbalimbali ya nchi, wizara hiyo ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Idadi ya wasichana wanaojifunza Qur'ani Tukufu kupitia kozi za majira ya joto ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wavulana, ilisema taarifa hiyo..

Kozi hizo za Qur'ani zinafanyika katika misikiti, vituo vya kidini na maeneo mengine, wizara ilibainisha.

Likizo za msimu wa joto hutoa fursa nzuri ya kueneza elimu ya Qur'ani miongoni mwa wanafunzi, maafisa wa wizara hiyo wanasisitiza.

Wizara ya Wakfu hapo awali ilitangaza kushiriki kwa zaidi ya watoto 50,000 wa familia za wahamiaji katika kozi za Qur'ani za majira ya joto nchini Algeria.

Algeria ni nchi iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

 4230638

captcha