IQNA

Wafungwa 600 wahifadhi Qur'ani Dubai

12:59 - January 13, 2022
Habari ID: 3474801
TEHRAN (IQNA)- Wafungwa wapatao 608 huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Idara ya Magereza Dubai imesema katika mwaka wa 2021, wafungwa 1,228 walishiriki katika mipango mbali mbali ya kielimu, kidini, kimichezo na kitaalamu.

Katika mpango wa kuwahimiza wafungwa Waislamu wahifadhi Qur'ani Tukufu kwa viwango mbali mbali, idadi ya waliohifadhi Qur'ani mwaka 2021 ilikuwa ni 275 na waliohifadhi Qur'ani mwaka 2020 walikuwa ni 333 na hivyo kufanya idadi ya waliohifadhi Qur'ani katika kipindi cha miaka miwili kuwa ni 608.

Aidha wafungwa wengi wameweza kumaliza masomo ya kiakademiki katika viwango mbali mbali kwa kushirikiana na Idara ya Elimu Dubai pamoja na vyuo vya kimataifa na kimataifa.

Wafungwa Dubai pia wameweza kupata masomo ya taalauma mbali mbali kama vile utenenezaji filamu, lugha ya Kiingereza, Kichina na saikolojia.

3477355

captcha