IQNA

22:02 - May 04, 2022
Habari ID: 3475205
TEHRAN (IQNA)- Makaburi ya Waislamu na Wakristo wa Kiothodoxi yamehujumiwa katika mji wa Malmo nchini Sweden katika kile kinachoonikana na kuongezeka chuki zinazochochewa na makundi ya wazungu wenye misimamo mikali ya kibaguzi.

Taarifa zinasema makaburi 20 ya Waislamu na Wakristo Waothodoxi yalihujumiwa katika Maziyara ya Ostra  katika mji wa Malmo kusini mwa Sweden.

Makaburi ya hayo yalipakwa rangi nyekundu na watu wasiojulikana na polisi wameanzisha uchunguzi huku utambulisho wa waliotekeleza uhalifu huo ukiwa bado haujabainika.

Hayo yanajiri wakati ambao Sweden hivi karibuni imeshuhudia kitendo kiovu cha kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu na mwanasiasa mwenye misimamo mikali ya kibaguzi.

3478762

Kishikizo: sweden ، waislamu ، makaburi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: