IQNA

Mpango wa Makuburi makubwa zaidi ya Waislamu Ulaya

20:37 - November 26, 2021
Habari ID: 3474602
TEHRAN (IQNA)- Kumezinduliwa mpango wa kujenga makaburi makubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya huko Uingereza katika eneo eneo la Blackburn, Lancashire.

Mradi huo ambao ni muhimu sana kwa jamii ya Waislamu unafadhiliwa na mandugu wa Issa ambao ni mabilinea mashuhuri nchini Uingereza.

Makaburi hayo ya Waislamu ambayo yamepewa jina la Bustani ya Makumbusho ya Issa yako katika eneo lenye ukubwa wa ekari 85. Inakadiriwa kuwa eneo hilo litakuwa na ploti 35,000 za makaburi.

Aidha eneo hilo jipya la kuwazika Waislamu litakubwa kubwa kuliko makaburi  ya Waislamu yajulikanayo kama ‘Bustani ya Amani’ huko East London lenye makaburi 10,000 ambayo yote yamejaa.

Mpango wa kujenga makaburi hayo ya Waislamu Uingereza umekuja kufuatia ongezeko la vifo vitokanavyo na COVID-19.

3476658

Kishikizo: uingereza ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha