IQNA

Wapalestina wakumbuka siku ya Maafa Makuu maarufu kama Siku ya Nakba

22:21 - May 16, 2022
Habari ID: 3475260
TEHRAN (IQNA)- Miaka 74 iliyopita, utawala bandia wa Israel ulitangaza uwepo wake baada ya kufanya mauaji makubwa ya umati dhidi ya Wapalestina. Siku hii inajulikana kama Siku ya Nakba.

Tarehe 14  Mei inasadifiana na mwaka wa 74 wa kufukuzwa mamia ya maelfu ya Wapalestina kwenye ardhi zao na  tarehe 15 Mei, utawala pandikizi wa Kizayuni uliopachikwa jina bandia la Israel, utatimiza miaka 73 tangu kupandikizwa kwake kwenye ardhi hizo za Wapalestina. Siku hii ya kutimuliwa Wapalestina katika ardhi zao inajulikana kama Siku ya Nakba yaani Siku ya Maafa Makuu. Ikumbukwe kuwa Wapalestina zaidi ya 750,000 walitimuliwa kutoka ardhi zao mwaka 1948 wakati wa kuundwa dola haramu la Israel na hivyo wakasambaratika katika kambi za wakimbizi huko Ghaza, Ukingo wa Magharibi, Syria, Jordan, Lebanon na maeneo mengine duniani. Hivi sasa kunakadiriwa kuwepo wakimbizi zaidi ya milioni tano Wapalestina duniani. 

Kabla ya kuundwa utawala bandia wa Israel, askari wa Uingereza waliikalia kwa mabavu Palestina kufuatia kushindwa utawala wa Othmania wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Miaka mitano baadaye Jumuiya ya Kimataifa iliikabidhi Palestina kwa Uingereza na kuiweka chini ya mamlaka ya mkoloni huyo.

Kishikizo: nakba palestina israel
captcha