IQNA

Waislamu na siasa Ulaya
22:10 - May 23, 2022
Habari ID: 3475285
TEHRAN (IQNA) - Akhtar Zaman amechaguliwa kama meya mpya wa mji wa Bolton nchini Uingereza, na kuwa Muislamu wa kwanza anayechukua nafasi hiyo.

Zaman, ambaye ni diwani wa Halliwell, alichukua jukumu hilo Jumatano kutoka kwa Meya anayemaliza muda wake Linda Thomas.

Akiongea katika sherehe iliyojaa hisia, meya mpya Muislamu alisema jukumu jipya ni kilele cha safari ndefu ambayo ilianza katika kijiji kidogo huko Pakistan.

Akinukuu mistari ya mashairi ambayo baba yake alimtuma kama kijana, Diwani Zaman alisema: "Nimetoa damu yangu kwa uboreshaji wa bustani hii ya maua, nikumbuke wakati machipuo yatakapowadia."

Alipomaliza hotuba yake, alimshukuru tena baba yake marehemu, na kuongeza: "Sasa msimu wa machipuo umewadia."

Diwani Zaman alipendekezwa kwa jukumu hilo na kiongozi mpya wa baraza la mji Martyn Cox.

Pendekezo hilo liliungwa mkono na Meya wa zamani Diwani Martin Donaghy ambaye alisema amefanya hivyo kwa fahari kamili."

Alisema: "Ikiwa unahitaji rafiki, Akhtar yuko hapa kwa ajili yako." Diwani Donaghy ameongeza kuwa meya mpya "amekuwa akipinga ubaguzi wowote ule."

3479026

 

Kishikizo: muislamu ، meya ، bolton ، uingereza ، Akhtar Zaman
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: