IQNA

Ibada ya Hija

Msomi ahimiza kutumia Hija kukabiliana na uenezi wa chuki dhidi ya Uislamu

15:35 - July 10, 2022
Habari ID: 3475484
TEHRAN (IQNA) – Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa Tehran ameungumzia utambulisho wa amani wa Ibada ya Hija na kusema nukta hii inapaswa kutumiwa kukabiliana na propaganda za chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia zinazoenezwa na baadhi ya vyombo habari vya Magharibi.

Akizungumza na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) Ijumaa, Hujjatul-Islam Mohammad Hassan Aboutrabi Fard alipongeza utendaji wa Waislamu katika ibada ya Hija hasa kwa kuzingatia washiriki ni kutoka kaumu mbali mbali.

"Moja ya nembo muhimu za Hija ni kujenga jamii ambayo wanadamu kutoka kaumu na mataifa  tofauti kutoka ulimwenguni kote hukusanyika mahali salama kwa mujibu wa maadili yatokanayo na mafundisho ya kidini na kibinadamu na hufanya ibada yenye muelekeo wa kidini, kisiasa na kijamii kwa utaratibu na nidhamu kamili," amesema.

Ameitaja Hija kuwa ni fursa ya kukuza Uislamu zaidi, na kuongeza wamba jukumu la wasomi na viongozi wa Kiislamu ni kuelezea kuhusu misingi ya hali ya juu ya Hija  kwa ulimwengu na kwa kufanya hivyo, kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu katika vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na Kizayuni ambavyo vina bajeti maalumu ya kuwasilisha taswira potovu na isiyo sahihi ya Uislamu.

Hija ni moja wapo ya nguzo za Uislamu kwamba Waislamu ambao wana uwezo wanapaswa kutekeleza ibada hii angalau mara moja katika maisha yao. Waislamu kawaida huweka akiba kwa miaka kadhaa ili kushiriki katika ibada hiyo.

Hija inajumuisha ibada  ambayo huchukua  zaidi ya siku tano katika mji mtakatifu zaidi wa Kiislamu Makka, na maeneo ya karibu ya Saudi Arabia ya Magharibi.

4069064

captcha