IQNA

Uzayuni na Marekani

Taarifa ya Hamas kuhusu safari ya Biden Asia Magharibi

12:18 - July 14, 2022
Habari ID: 3475502
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaja safari ya Rais Joe Biden wa Marekanii katika eneo la Asia Magharibi (Mashariaki ya Kati) kuwa ni kielelezo cha kivitendo cha uungaji mkono kamili wa Washington kwa Tel Aviv na imeonya kuhusu hatari ya safari hiyo kwa eneo hilo na mapambano ya Palestina.

atika safari yake ya kwanza eneo la Asia Magharibi akiwa Rais wa Marekani, Joe Biden, aliwasili Tel Aviv jana Jumatano (Julai 13), na baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa utawala wa ya Kizayuni wa Israel, alitarajiwa kukutana na Mahmoud Abbas, mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Baadaye ataelekea Jiddah nchini Saudi Arabia ambako atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo. 

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetoa taarifa na kuitaja safari hiyo kuwa inaonesha upendeleo wa wazi wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni na kwamba inafunika jinai za Tel Aviv, zikiwemo mauaji, kuwafukuza Wapalestina katika makazi yao, ubaguzi wa rangi, ujenzi wa vitongoji vya walowezi kaika ardhi iliyoghusubiwa na mpango wa Kuzayunisha ardhi ya taifa la Palestina na maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo.

Taarifa ya Hamas imesema: Tunaitaka serikali ya Marekani iache kudharau na kupuuza haki thabiti za watu wa Palestina na kuacha kuupendelea utawala wa kikatiili wa Israel.  

Mwishoni mwa taarifa yake, Hamas imetahadharisha kuhusu hatari ya mipango ya safari ya Biden katika eneo la Magharibi mwa Asia na juhudi zake za kutaka kuuunganisha utawala wa Kizayuni katika nchi za eneo hilo na kupanua wigo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya nchi za Kiarabu na utawala huo haramu.

Ziara ya Rais wa Marekani nchini Saudi Arabia na Israel imeambatana na ukosoaji mkubwa wa ndani ya Marekani na wa mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kupuuza ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika huko Israel na Saudi Arabia.

Wanaharakati wa Kipalestina wametoa wito wa kufanyika maandamano makubwa kulaani ziara ya Rais wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Maandamano hayo yatakayoanza leo Alkhamisi katika uwanja wa al Manara mjini Ramallah yataelezea misimamo ya upinzani ya wananchi wa Palestina dhidi ya sera za Marekani za kuuunga mkono utawala vamizi wa Israel.

Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas)  amesisitiza katika taarifa hiyo kwamba, ziara ya Rais wa Marekani inalenga kuzidisha migawanyiko na hitilafu katika eneo la Magharibi mwa Asia, kuunda miungano mipya ya kutetea mradi wa Kizayuni na siasa za kupenda kujitanua za utawala haramu wa Israel na kukandamiza harakati hai za wananchi wa Palestina.

4070700

captcha