IQNA

Uchambuzi wa kisiasa

Safari ya Biden Asia Magharibi ni muendelezo wa ubeberu wa Marekani

16:05 - July 11, 2022
Habari ID: 3475490
TEHRAN (IQNA)- Mbali na kukosolewa sana safari yenye malengo ya kibeberu ya Rais Joe Biden wa Marekani huko Saudi Arabia na vilevile katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia na kuitwa Israel, lakini kile kinachodhihirika zaidi katika ukosoaji huo ni kuwa kufanyika safari hiyo sambaba na siku za kutekelezwa ibada tukufu ya Hija ni jambo ambalo haliwezi kuwa limefanyika hivi hivi bali limepangwa kufikia malengo maalumu.

Biden anatarajiwa kutembelea eneo la Asia Magharibi kuanzia 13 hadi 16 Julai katika safari ambayo inatajwa kuwa na malengo ya kujitanua Marekani na pia kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mipango hiyo ya kibeberu ya Marekani inafuatiliwa na wapangaji wa njama ya kufanikisha mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kati ya nchi za Kiarabu na Kiislamu za Asia Magharibi na utawala ghasibu wa Israel na apatano yoyote yatakayofikiwa kati ya pande hizo yafanyike katika fremu ya kile kinatajwa kuwa Mapatano ya Abraham.

Kwa mujibu wa mpango wa amani uliowasilishwa na Amir Abdallah, mrithi wa wakati huo wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na kupitishwa katika kikao cha viongozi wa nchi za Kiarabu mnamo mwaka 2000 mjini Beirut Lebanon, kuanzishwa uhusiano wowote kati ya nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kulishurutishwa na kuundwa serikali huru ya Palestina ambayo ingekuwa na mji mkuu wake huko Beitul Muqaddas, ambapo pia utawala huo ghasibu ulitakiwa kuondoka katika ardhi nyingine za Waarabu kwa mujibu wa maazimio nambari 242 na 338 ya Baraza la Usalama la Umaoja wa Mataifa.

Uhusiano wa kawaida na utawala wa kibaguzi wa Israel

Pamoja na hayo lakini duru mpya ya mazungumzo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida wa nchi za Kiarabu na utawala huo wa kibaguzi ulianzishwa katika kipindi cha utawala wa Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani, katika hali ambayo utawala huo haramu si tu ulikuwa umepuuza sharti hilo muhimu la nchi za Kiarabu bali uliendelea kuteka na kukalia kwa mabavu ardhi zaidi za nchi za Kiarabu na kuziunganisha rasmi na ardhi za Wapalestina zilizoghusubiwa mwaka 1948. Ardhi hizo ni pamoja na za milima ya Golan ya Syria na vilevile vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Pastina.

Wakati huo huo Marekani ilipuuza ahadi ilizotoa huko nyuma kuhusiana na kadhia ya Palestina kwa kuamua kuuhamishia ubalozi wake Beitul Muqadda kutoka Tel Aviv.

 

Wananchi wanapinga uhusiano na Israel

Kwa kutilia maanani ukiukaji huo wa wazi wa sheria za kimataifa na mapatano yote yaliyokuwa yamefikiwa huko nyuma, mazungumzo na mapatano ya hivi sasa yametakiwa yafanyike chini ya anwani ya 'Mapatano ya Ibraham (Ibrahim)' ili yapate kukubalika mbele ya fikra za waliowengi katika nchi za Kiarabu na Kiislamu. Suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa wapangaji wa mapatano mapya ya Waarabu na Israel kwa kadiri kwamba licha ya kuwepo mikataba kama hiyo ya amani kati ya utawala huo ghasibu na baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Misri, lakini uhusiano huo haukubaliki mbele ya wananchi wa nchi za Kiarabu. Kwa maana kuwa hata kama nchi hizo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo wa Kizayuni lakini usalama wake bado haujadhaminiwa katika mazingira ya kawaida na ndio maana balozi za utawala huo zimefunguliwa katika ghorofa za juu kabisa katika majengo ya kibiashara. Mifano ya wazi ya ukweli huo inaonekana nchini Misri na Bahrain ambayo imeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo hivi karibuni.

Chaguo gumu kwa watawala wa Saudia

Katika uwanja huo, hali ya mambo ni ngumu kwa Saudi Arabia ambayo ilianzisha mpango wa awali wa kuwa na uhusiano na utawala wa kibaguzi wa Israel na ambao wakati huo huo unajichukulia kuwa kinara wa ulimwengu wa Kiislamu. Kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja na wa wazi na Israel ni chaguo gumu kwa watawala wa Saudia ambao hata hivyo wamekuwa na uhusiano wa siri wa miaka mingi na Wazayuni.

Katika upande wa pili Tel Aviv inaishinikiza Saudia iweke wazi uhusiano huo haraka iwezekanavyo ili kuzishawishi nchi nyingine za Kiarabu zifuate mkondo huo.

Safari ya Biden katika msimu wa Hija

Moja ya njama zionazofanyika katika uawanja huo ni kufanyika wakati mmoja safari ya Joe Biden huko Israel na Saudi Arabia tena katika msimu wa Hija, ili hilo litajwe kuwa ni katika mkondo wa kufanikisha Mapatano ya Abraham.

Pamoja na hayo lakini kuna uwezekano wa njama hiyo kuwa na matokeo kinyume na wanavyotarajia wapangaji wake kwa sababu ni wazi kuwa wanataka kutumia vibaya msimu wa Hija kwa maslahi yao ya kisiasa. Kwa msingi wa njama hiyo hatari, utawala wa Kizayuni unapanga kufutilia mbali uwezekano wa kubuniwa serikali huru ya Palestina tena kwa msaada wa nchi vibaraka za Kiarabu na Kiislamu, nayo serikali ya Jeo Biden inapanga kupora na kutumia fedha za mafuta za Saudi Arabia kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na vita vya Ukraine.

4069996

Kishikizo: biden israel
captcha