Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), lilitabiri kuwa Biden atakaa kimya tena baada ya Israel kuripotiwa kuwachinja watoto 50 wa Kipalestina huko Gaza kwa silaha zilizotolewa na Marekani.
Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya majengo mawili ya ghorofa ya makazi ya familia ya Shalayel na al-Ghandour kaskazini mwa Gaza, huku 50 kati ya waliokufa wakiwa watoto.
Mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza yanakuja wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiwaua takriban watu 52 kaskazini mashariki mwa Lebanon.
Israel imeua zaidi ya watu 43,000 huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto Wapalestina, na takriban watu 2,900 wameuawa na Israel huko Lebanon.
Katika taarifa, CAIR, yenye makao yake makuu Washington, D.C. ilisema:
"Wakati Israel inawachinja tena watoto wa Kipalestina kwa kutumia silaha zinazotolewa na walipa kodi wa Marekani, tunatabiri kwa masikitiko kwamba utawala wa Biden utakaa kimya na badala yake utaendelea na ushirikiano wake na mauaji ya kimbari ya serikali ya mrengo wa kulia ya Israel, mauaji ya kikabila, uharibifu mkubwa na njaa ya kulazimishwa. Ushirikiano huu wa vitendo na uhalifu dhidi ya ubinadamu unafanyika kwa lengno la kudhoofisha utu wa Wapalestina na kampeni ya miongo mingi ya kupinga Uarabu, Uislamu na Palestina ambayo ilifanya udhalilishaji huo uwe lazima.
Siku ya Alhamisi, CAIR ililaani jaribio la Rais wa zamani Bill Clinton "la matusi na chuki dhidi ya Uislamu" la kuhalalisha mashambulizi yanayoendelea ya utawala wa Israel dhidi ya raia wa Palestina huko Gaza.