IQNA

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon

Mapambano yamesambaratisha mpango wa Marekani wa 'Mashariki ya Kati Mpya'

11:46 - July 14, 2022
Habari ID: 3475500
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, mojawapo ya matunda muhimu zaidi ya mhimili wa Muqawama au mapambano ya Kiislamu yalikuwa ni kuuzima mpango wa Marekani wa kuanzisha Mashariki ya Kati Mpya.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Hizbullah katika vita vya mwaka 2006 dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Sayyid Nasrallah ameongeza kuwa, moja ya matokeo muhimu zaidi ya Vita vya Siku 33 yalikuwa ni kuanzisha mlingano wa kuzuia hujuma za adui mzayuni dhidi ya Lebanon.

Katibu Mkuuu wa Hizbullah amefafanua kwa kusema: kwa rehma za Mwenyezi Mungu mkakati wa mlingano wa kuzuia hujuma unamfanya adui Israel afikirie mara elfu kuanzisha chokochoko yoyote ya kijeshi dhidi ya Lebanon.

Nasrullah amebainisha kuwa suhula ulizonazo muqawama hii leo hazijawahi kushuhudiwa mfano wake hapo kabla na azma na irada yake ya kupigana vita ni imara zaidi kuliko ilivyowahi kuwa wakati wowote ule.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameendelea kueleza kwamba, muqawama ndio nguvu pekee inayoweza kutumiwa na Lebanon kuzifikia maliasili zake za mafuta na gesi na kuweza kuzichimba na kwamba uchimbaji wa nishati hizo ni fursa ya kipekee ya kuiokoa Lebanon na serikali yake.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Sayyid Hassan Nasrallah ameizungumzia pia Marekani na kueleza kwamba Marekani ya leo ni tofauti sana na ya mwaka 2003 na 2006 na kwamba rais aliyezeeka wa nchi hiyo anaakisi taswira halisi ya Marekani yenyewe ambayo imeingia kwenye awamu ya uzee.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ametanabahisha pia kuwa, hivi sasa kuna nakala nyingine mpya inayoandaliwa ya mradi wa kuanzisha Asia ya Magharibi Mpya; na safari ya Joe Biden katika eneo hili inafanyika katika muelekeo huo pia.

3479695

captcha