IQNA

Haraakti za Qur'ani

Maonyesho ya Qur’ani Tukufu yainduliwa Asir, Saudia

23:28 - August 12, 2022
Habari ID: 3475614
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho yanayohusiana na sekta ya uchapishaji Qur’ani Tukufu yamefanyika katika mji wa Asir nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu taarifa, maonyesho hayo yanaonyesha shughuli za Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd.

Wanaotembelea maonyesho hayo wanashuhudia mchakato  mzima wa uchapishaji na usambazwaji Qur’ani Tukufu pamoja na teknolojia inayotumika katika uchapishaji.

Maonesho hayo ambayo yamezinduliwa Alhamisi na Idara ya Masuala ya Kidini ya Asir yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa siku 10.

Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd kiko katika mji wa Madina na mbali na Misahafu ya Kiarabu pia huchapisha tarjuma za Qur’ani kwa lugha 40. Kituo hicho huchapisha Misahafu karibu milioni 10 kwa mwaka.

Quran Printing Industry Expo Opens in Asir

Quran Printing Industry Expo Opens in Asir

3480058

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha