Kulingana na wizara hiyo, shindano hilo litafanyika katika sehemu tofauti za wavulana na wasichana.
Kategoria za shindano hilo ni pamoja na Tajweed, tafsiri ya Qur'ani na kusoma Juzuu tofauti za Kitabu Kitakatifu.
Washiriki wanahitaji kuwa raia wa Saudi Arabia na kiwango cha juu cha umri ni miaka 18 kwa baadhi ya kategoria na 24 kwa zingine.
Washindi watapata zawadi za pesa taslimu za hadi riyal milioni mbili za Saudia, wizara iliongeza.
Mashindano hayo yanayojulikana kama Tuzo ya Qur'ani ya Mfalme Salman, huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo.
Inalenga kukuza shughuli za Qur'ani nchini katika viwango tofauti, kulingana na waandaaji.
3490028