IQNA

Nakala 50,000 za Qur'ani Tukufu zasambazwa katika Msikiti wa Makka Mwezi wa Ramadhan

17:48 - May 01, 2022
Habari ID: 3475194
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya Misahafu 50,000 imesambwazwa kwa waumini waliofika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haram kwa ajili ya Umrah au Hija ndogo wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hamza bin Ibrahim al-Salemi, mkuu wa Idara ya Nakala za Qur'ani Tukufu amesema mpango wa usambazaji huo ni sehemu ya ubunifu uliopewa jina la 'Msahafu kwa Kila Mwenye Kutekeleza Umrah'.

Aidha amesema idara yake imechunguza Misahafu yote katika Msikiti Mtakatifu kuhakikisha kuwa ni ile iliyoidhinsihwa na Kituo cha Kuchapisha Qur'ani cha Mfalme Fahd. Afisa huyo amebaini kuwa ndani ya Al Masjid Al Haram kuna Misahafu 150,000.

Wakati huo huo, Taasisi ya Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina imesema lita milioni mbili za maji ya Zamzam zimesambazwa miongoni mwa waumini katika misikiti hiyo wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

4054021

 

Kishikizo: qurani tukufu makka
captcha