IQNA

Qur'ani Tukufu

Zaidi ya nakala milioni 300 za Qur'ani zimechapishwa Madina katika miongo minne

15:34 - October 27, 2024
Habari ID: 3479653
IQNA - Zaidi ya nakala milioni 300 za Qur'ani Tukufu zimechapishwa katika Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd mjini Madina, Saudi Arabia.

Kituo hicho kina nakala asili tano za Misahafu iliyoandikwa kwa mkono na kuidhinishwa na kamati yake ya kisayansi.

Nakala mbili kati ya hizo zimo katika riwaya za Hafs na nyingine tatu katika riwaya za Warsh, al-Dawri na Qalun.

Timu ya wanazuoni na wataalamu wa Kiislamu wanasahihisha kwa makini kila toleo baada ya maandishi kukamilika kabla ya Kurani kuchapishwa.

Pia kuna mfumo maalum uliowekwa wa kufuatilia hatua zote za uchapishaji wa Qur'ani Tukufu.

Nyingi za nakala zilizochapishwa na taasisi hiyo ni pamoja na tafsiri za Qur'ani Tukufu katika lugha mbalimbali.

Hadi sasa, imechapisha tafsiri za Qur'ani Tukufu katika lugha 72, zikiwemo 39 zinazozungumzwa Asia, 16 zinazozungumzwa Ulaya, na lugha 19 za Kiafrika.

Mbali na Qur'ani, kituo hicho kinachapisha vitabu vya sayansi ya Qur'ani na tafsiri za vitabu mbalimbali vya Qur'ani na vya Kiislamu.

Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd kilizinduliwa katika mji mtakatifu wa Madina tarehe 30 Oktoba 1984, na mtawala wa wakati huo wa Saudi Arabia Mfalme Fahd bin Abdul Aziz na hadi leo ni kituo kikubwa zaidi cha uchapishaji wa Qur'ani duniani.

4244344

 

Habari zinazohusiana
captcha