Katika ziara hiyo ya Jumatatu, balozi wa Iran na ujumbe wake walifahamishwa kwa kina shughuli za kituo hicho, ambapo walitazama hatua mbalimbali za uchapishaji wa Qur'ani na teknolojia inayotumika katika mchakato huo.
Enayati alipongeza juhudi na kujitolea kiwanda hicho katika kuchapisha nakala za Qur’ani Tukufu.
Kituo cha Uchapishaji Qu’ani cha Mfalme Fahd, lililoko Madina, linasifika kwa utayarishaji wake wa kina wa Qur’ani Tukufu.
Kituo cha Uchapishaji Qu’ani cha Mfalme Fahd kilianzishwa mwaka wa 1984, na huchapisha takriban nakala milioni 10 za Qur’ani kila mwaka, na nakala hizo hujumuisha tafsiri katika lugha nyingi kama vile Kiingereza, Kiindonesia, Kirusi, Kijapani, Kiajemi, Kiurdu, Kiswahili, Kibengali na Kikorea.
3490391