IQNA

Saudia imechapisha nakala milioni moja mpya za Qur'ani kwa lugha 10

12:49 - June 12, 2021
Habari ID: 3474000
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Masuala ya Kiislamu katika Ufalme wa Saudi Arabia imetangaza ksambaza nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu ambazo zimetarjumiwa kwa lugha 10. 
Taarifa ya wizara hiyo imesema misahafu hiyo imechapishwa hivi karibuni kwa ushirikiano na Kituo cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur'ani Tukufu.
Imedokezwa kuwa mishahafu hiyo imesambazwa katika vituo 413 vya Kiislamu katika maeneo mbali mbali duniani. 
Abdullatif bin Abdulaziz Al-Sheikh, Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia amesema usambazwaji misahafu hiyo ni muhimu katika kustawisha uelewa wa Qur'ani miongoni mwa vijana.
Kishikizo: qurani tukufu ، saudia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :