IQNA

Waislamu wa Oman

Msikiti Mkubwa Zaidi wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Wazinduliwa nchini Oman

19:47 - November 23, 2022
Habari ID: 3476137
TEHRAN (IQNA) - Msikiti mkubwa zaidi wa Oman kwa Waislamu wa Madhehebu ya Shia ulizinduliwa katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu, Muscat.

Waziri wa Wakfu Mohammed Said al-Ma’amari na Ayatullah Muhsin Araki, mjumbe wa Baraza Kuu la Hauza (vyuo vikuu vya Kiislamu ) Iran, walikuwa miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.

Pia kulikuwa na wanazuoni na maulamaa wa madhehebu ya Shia na Sunni kutoka Oman na nchi nyingine za Kiarabu.

Msikiti wa Jami al-Salam huko Muscat umejengwa kwenye eneo la ardhi la mita za mraba 30,000 na eneo lake la ujenzi lenye ukubwa wa mita za mraba 12,820.

Idara ya Wakfu katika eneo la Al-Lawatia ndiyo iliyoidhinisha  ujenzi wa msikiti huo.

Katika hafla nyingine iliyofanyika msikitini hapo Jumanne jioni, kitabu cha Ayatullah Araki kuhusu hadhi ya misikiti katika Fiqh ya Kiislamu kilizinduliwa mbele ya Mkuu wa Idara ya Wakfu  huko Al-Lawatia, Balozi wa Iran nchini Oman na baadhi ya maulamaa wa Kishia na Kisunni nchini Oman.

Ayatullah Muhsin Araki ni mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Iran na aliwahu kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.

Oman ni nchi iliyoko Kusini Magharibi mwa Asia, ikipakana na Bahari ya Arabia, Ghuba ya Oman, na Ghuba ya Uajemi, kati ya Yemen na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Takriban Waomani wote ni Waislamu.

4101586

 

captcha