IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Muscat Mwenyeji wa Mashindano ya Qur'ani ya Vikosi vya Wanajeshi wa Oman na Iran

17:41 - June 05, 2024
Habari ID: 3478937
IQNA - Mashindano ya Qur'ani kati ya majeshi ya Iran na Oman yanaendelea katika mji mkuu wa Oman, Muscat.

Hili ni toleo la kumi la mashindano hayo na Ilianza Juni 3 na linahitimishwa  leo, Juni 5.
Washindani wameshindana katika kuhifadhi Qur'ani katika ngazi nne: Kuhifadhi Qur'ani Tukufu, na kuhifadhi Juzuu 18, 10 na 5 za Qur'ani Tukufu
Kuna washiriki wanne kutoka Iran na wanne kutoka Oman katika kila kategoria, kulingana na Seyed Mehdi Gatmirian, mkuu wa timu ya Iran iliyotumwa Oman.
Wahifadhi wa Irani wanatoka Jeshi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Polisi, na Wizara ya Ulinzi, alisema.
Amebainisha kuwa, wataalamu wa Qur'ani wa Iran Karim Dolati na Mutaz Aqaei ni wajumbe wa jopo la majaji katika mashindano hayo.
Amesema mashindano hayo yana lengo la kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya majeshi ya nchi hizo mbili kupitia shughuli za Qur'ani na kwa kuzingatia Aya ya 103 ya Surah Al Imran "Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msitawanyike."
4219906

Habari zinazohusiana
captcha