IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wananchi wamekuwa ndio "mashujaa wakuu wa historia ya Mapinduzi"

20:37 - August 30, 2022
Habari ID: 3475703
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: katika matukio yote yaliyojiri, wananchi wamekuwa ndio "mashujaa wakuu wa historia ya Mapinduzi" na ukweli huo unatoa somo na mazingatio na kuwaonyesha viongozi wote ni namna gani inapasa waamiliane na wananchi hao.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo katika mkutano na Rais na mawaziri wa serikali yake, ambapo mbali na kuashiria taufiki na mafanikio iliyopata serikali katika kipindi cha mwaka mmoja, ameshauri mambo muhimu kadhaa kikiwemo kipaumbele cha suala la uchumi na akaongezea kwa kusema: "msisimko wa taifa zima katika zama za Mapinduzi", "mshangao uliopata Uistikbari katika kukabiliana na adhama ya Mapinduzi", "uadui usio na mwisho wa watumiaji mabavu duniani", "kutokuwa na ulinzi nchi na mji mkuu wa kujihami na mashambulizi ya anga ya Saddam", "kujifaragua magaidi nchini kote na kukosekana usalama katika miaka ya kwanza ya Mapinduzi, "utendaji wa serikali na mabunge mbalimbali baada ya Mapinduzi", "ushiriki wa kipekee wa wananchi katika hamasa ya Kujihami Kutakatifu na katika medani zingine za kukabiliana na maadui” na “ushiriki usio na ajizi na unaostahiki pongezi wa wananchi katika maandamano na shughuli mbalimbali” ni miongoni mwa masuala ambayo kumbukumbu zake inapasa zidumu na kubakia hai katika fikra za jamii.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kufufua matumaini na imani ya wananchi ndiyo taufiki muhimu zaidi iliyopata serikali; na akaongezea kwa kusema: "wananchi wanaiona serikali iko katikati ya medani ikishughulika kuchapa kazi na kufanya juhudi ili kutatua matatizo na kuwafikishia wao huduma; na huu ni ukweli, kwamba wamefufua kwa kiwango kikubwa matumaini na imani ya umma; na hapana shaka, jitihada hizi zimefanikiwa katika baadhi ya maeneo, na katika baadhi ya maeneo, bado hazijawa na tija inayotakiwa."

 
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei amesema "kuitoa jamii kwenye hali ya kutegemea maamuzi na hatua zitakazochukuliwa na wengine", "kuiepusha nchi na ushurutishwaji" na "kuupa umuhimu uwezo wa ndani" ni miongoni mwa mafanikio iliyopata serikali.
Aidha amesema, serikali ya 13 ni ya "uwajibikaji" na akaeleza kwamba: "mielekeo mizuri iliyoonyeshwa katika uga wa sera za nje na utamaduni", na "kuzipa uzito kaulimbiu za Mapinduzi zikiwemo za kutetea uadilifu, kuunga mkono wanyonge, kujiepusha na uashrafu na ubwanyenye na kupiga vita Uistikbari ni miongoni mwa nukta zingine za mafanikio iliyopata serikali.
4081905
captcha