IQNA

Fikra za Kiislamu

Sifa tano za jamii inayofaa kwa mujibu wa Qur'ani

14:39 - September 08, 2022
Habari ID: 3475751
TEHRAN (IQNA) – Jamii ya Qur’ani inapaswa kuwa na seti ya vipengele na muhimu zaidi ni pamoja na imani, akili, elimu, uadilifu, na wema au ukarimu.

Mitume wote walikuja na lengo moja nalo lilikuwa ni kuwaongoza wanadamu kuelekea kwenye ubora na ukamilifu na kuanzishwa kwa jamii inayohakikisha usalama na uadilifu. Mitume wametoa mipango na nukta mbalimbali ili kuwaongoza watu katika njia hii.

Uislamu pia umetoa mapendekezo yake ambayo yametajwa ndani ya Qur'ani na viongozi wake pia.

Kwa mujibu wa Qur'an, jamii inayofaa inapaswa kuwa na vipengele kadhaa na utambuzi wao utapelekea ustawi kwa watu binafsi. Zifuatazo ni sifa muhimu zaidi za jamii inayofaa kwa mujibu wa Qur'an:

Imani: Imani ni kipengele muhimu zaidi cha jamii ya Qur'ani. Kwa kuzingatia Quran, hatua za mwanzo katika njia ya uongofu ni kuikubali dini na kuamini mambo ya ghaibu kama vile Mwenyezi Mungu, Malaika, Akhirah, Ma’ad. Lakini imani hii pekee haitoshi, badala yake, kila mtu au jamii inapaswa kupitia mitihani migumu ili ibainike ni kwa kiasi gani wanashikamana na imani zao.

Akili: Jumuiya ya kidini ni jamii ya wasomi. Ufahamu huu unamaanisha kutumia hekima katika mambo yote ya maisha. Akili hairuhusu ndoto na majaribu kutawala jamii na itajaribu kuzuia kupotoka.

Ujuzi: Jamii inayofaa haitachukua hatua yoyote kamwe bila kuwa na maarifa ya hapo awali ili jamii isielekezwe kwenye ujinga. Kwa hakika jamii inayoweka akili pembeni itaishia kwenye ujinga.

Uadilifu: Uadilifu ndio njia ya karibu zaidi ya kufikia Taqwa au Kumcha Mungu. Kwa hiyo jamii ya kidini inayofaa haipendi haki tu bali pia inawaalika wengine kuizingatia na hata kujaribu kutetea haki za wanyonge.

Ukarimu: Jamii inayofaa itakuza wema katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Wanajamii watazingatia kipengele hiki hata katika maisha yao ya kibinafsi. Kinachoipa jamii uzuri ni sifa ya wema na ukarimu.

 

Na Hossein Allahverdi

captcha