IQNA

Netflix yaonywa kuhusu kukiuka maadili ya Kiislamu

18:50 - September 07, 2022
Habari ID: 3475747
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi limeilitaka shirika Netflix kuondoa maudhui ya kuudhi kwenye jukwaa lake la filamu.

Hatua ya kamati ya vyombo vya habari vya kielektroniki ya nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi iliangaziwa wakati wa mkutano wa Kamisheni Kuu ya Saudia ya Vyombo vya Habari vya Sauti na Picha.

Kamati ya baraza hilo ilikuwa imechukua uamuzi wa kuwasiliana na Netflix "kwa kuzingatia uchunguzi wa hivi majuzi kwamba jukwaa hilo lilikuwa likitangaza maudhui ambayo yanakiuka udhibiti kanini za nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi," taarifa ya tume ilisema.

“(Yaliyomo) yanakiuka maadili na kanuni za Kiislamu na za kijamii. Kwa hivyo, mfumo uliwasiliana ili kuondoa maudhui haya, ikiwa ni pamoja na maudhui yanayowalenga watoto, na kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa.”

Ilikubaliwa kuwa mamlaka za nchi wanachama zitafuatilia kuhukikisha kuwa Netflix kwa maagizo. "Ikitokea kwamba maudhui yanayokiuka yataendelea kupatikana, hatua muhimu za kisheria zitachukuliwa," taarifa hiyo iliongeza.

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi linaundwa na Saudi Arabia, Qatar, Imarati, Bahrain, Kuwait na Oman.

3480382

captcha