IQNA

Mfumo wa kifedha wa Kiislamu

Ripoti: Benki ya Kiislamu barani Afrika kustawi zaidi muongo ujao licha ya changamoto

13:17 - September 22, 2022
Habari ID: 3475822
TEHRAN (IQNA)- Rasilimali za benki za Kiislamu barani Afrika zinatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka 10 ijayo, kutokana na idadi kubwa ya Waislamu barani humo, shirika la taarifa za kifedha la Moody's Investors Service limebaini katika ripoti mpya.

"Kuna uwezekano mkubwa wa kukua katika sekta hii, kutokana na idadi kubwa ya Waislamu barani Afrika na mtajii mdogo wa kuanzia," alisema Mik Kabeya, Makamu wa Rais na mchambuzi mwandamizi wa Moody's.

Kwa mujibu wa baadhi ya takwimu, idadi ya Waislamu barani Afrika inafikia watu milioni 530, karibu 40% ya idadi ya Waafrika. Huko Afrika Kaskazini, idadi ya Waislamu ni zaidi ya 90%, karibu na viwango vya nchi za Ghuba ya Uajemi.

Idadi ya watu barani Afrika wasio na benki, hasa wale wanaojiondoa katika mfumo wa kawaida kwa sababu ya imani zao za kidini, wanawasilisha hifadhi na vitega uchumi visivyoweza kutumika.

Hata hivyo, changamoto zinazoendelea zitazuia ukuaji wa benki za Kiislamu katika kipindi cha miezi 12 hadi 18 ijayo.

Kuongezeka kwa ushindani miongoni mwa benki za kawaida barani Afrika kunaleta mazingira magumu katika benki ya Kiislamu.

Aidha, taratibu za kisheria, udhibiti na kodi kwa mfumo wa fedha wa Kiislamu katika bara zima ziko katika hatua za awali za maendeleo.

Rasilimali za benki za Kiislamu barani Afrika zilijumuisha 2% tu ya kimataifa na chini ya 10% ya jumla ya mali zote za benki za ndani katika nchi nyingi za Kiafrika kufikia Desemba 2021.

Hii ni licha ya kuwa, bara la  Afrika,  Kusini mwa Jangwa la Saharak, lina  karibu 15% ya idadi ya Waislamu duniani.

Hali hatahivyo ni tafauti nchini  Sudan, ambayo mfumo wake wa benki unafuata kikamilifu Shariah ya Kiislamu na Djibouti, ambapo mali ya benki ya Kiislamu ni karibu 25% ya mali ya sekta ya benki, ripoti hiyo ilisema.

3480587

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha