Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Afrika Kusini kimeanzisha kituo hicho, kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).
Ni kituo rasmi cha kwanza cha kufundisha Qur'ani kilichoanzishwa kama sehemu ya mpango wa Risalatallah.
Kitengo cha Kimataifa cha Qur’ani na Uenezi cha ICRO kinatekeleza mpango wa Risalatallah kwa lengo la kukuza harakati za Qur'ani za Iran katika ngazi ya kimataifa.
Idadi ya wanazuoni wa Kiislamu wa Shia na Sunni kutoka Iran na Afrika Kusini pamoja na shakhsia kadhaa wa Kikristo wa nchi hiyo ya Kiafrika walihudhuria sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Hikmat Dar-ol-Quran.
Akihutubu katika hafla hiyo, mwanazuoni wa ngazi za juu wa Iran Ayatullah Mahmoud Mohammadi Araqi ameitaja Qur'ani kuwa ni hazina ya kimaanawi kwa Waislamu na watu wengine duniani na kusema watu wanapaswa kurejelea Qur'ani kwa ajili ya kutatua masuala na kupata majibu ya maswali yao.
Quran Tukufu inatoa majibu kwa swali na changamoto yoyote, alisema.
Mwambata wa Utamaduni wa Iran, Mostafa Daryabari pia alitoa hotuba katika sherehe za uzinduzi huo na kusema, Kituo cha Hikmat Dar-ul-Quran kitashirikiana na vituo na misikiti tofauti ya kielimu na kidini nchini Afrika Kusini ili kushiriki nao hekima ya Qur'ani.
Ibrahim Buflu, mwanazuoni wa Afrika Kusini katika hotuba yake aliitaja Kituo cha Dar-ul-Quran kuwa ni zawadi kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Afrika Kusini na kusema mafundisho ya Qur'ani Tukufu, Mtume Mtukufu (SAW) na Ahl-ul-U. Bayt (AS) ni miongozo inayopaswa kufuatwa na wote ili kuepuka kupotoka.
3489821