IQNA

Bidhaa Halal

Makampuni ya Iran yashiriki Maonyesho ya Halal Uturuki + Video

22:45 - November 27, 2022
Habari ID: 3476159
TEHRAN (IQNA) – Maonesho ya 9 ya ‘Halal’ ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ambayo yamefanyika mjini Istanbul, Uturuki, kwa kushirikisha makampuni kutoka sehemu mbalimbali za dunia, yakiwemo makampuni 13 ya Iran ambayo yana msingi wa elimu au knowledge-based.

Wazalishaji wa bidhaa Halal kutoka nchi 30 za Kiislamu wameonyesha bidhaa na huduma zao za Halal katika hafla hiyo.

Makampuni ya Iran yameshiriki katika maonyesho hayo kwa uratibu wa Shirika la Kukuza Biashara la Iran na kwa ushirikiano wa idara ya masuala ya kimataifa ya Taasisi ya Viwango na Utafiti wa Viwanda ya Iran.

Yemen, Iraq na Algeria pia zimewakilishwa katika maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.

Nchi zilizoshiriki zinataka kuendeleza uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na kuimarisha uwekezaji na ushirikiano wa pande zote katika tasnia ya Halal, ambayo imekuwa na ukuaji wa kipekee katika miaka ya hivi karibuni katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu.

Soko la Halal la kimataifa, ikiwa ni pamoja na sekta ya fedha za Kiislamu, chakula, utalii, vipodozi, bidhaa za matibabu na nguo, lina thamani ya  dola trilioni 7 trilioni, kulingana na Baraza la Mkutano wa Halal Duniani.

Tukio hilo la siku nne limeoonyesha bidhaa na huduma mbalimbali zinazozingatia miongozo ya Kiislamu, yaani Halal, lilianza mjini Istanbul siku ya Alhamisi na limehitimishwa leo.

Mkutano wa 8 wa Halal wa Dunia pia ulifanyika katika mji wa Uturuki pamoja na maonyesho ya Halal. Mkutano huo ulijumuisha vikao vinavyojadili viwango vya Halal na njia za kukuza biashara ya Halal katika ulimwengu wa Kiislamu.

Katika ujumbe uliosomwa kwenye sherehe za ufunguzi, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipongeza kuongezeka kwa umaarufu wa soko la Halal kimataifa.

Alisema soko la Halal haliene tu miongoni mwa Waislamu bali pia limewavutia wengi wanaotaka bidhaa na huduma bora.

4102431

Kishikizo: bidhaa halala ، msingi wa elimu ، OIC
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha