IQNA

Wanawake Waislamu

OIC yaandaa Mkutano wa Kimataifa wa: 'Wanawake katika Uislamu: Hadhi na Uwezeshaji'

14:56 - November 06, 2023
Habari ID: 3477848
MECCA (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeandaa mkutano wa kimataifa wa siku tatu huko Jeddah unaoitwa "Wanawake katika Uislamu: Hadhi na Uwezeshaji" unaoanza Jumatatu.

Tukio hili ni maalum kwa ajili ya kukumbuka mafanikio ya ajabu ya wanawake wa Kiislamu katika historia na kukuza uelewa wa kina wa michango yao.
Malengo makuu ya mkutano huo yanajumuisha kuangazia majukumu makubwa yanayotekelezwa na wanawake katika maendeleo ya nchi wanachama wa OIC, kukabiliana na dhana potofu na simulizi hasi ambazo mara nyingi huonyesha dini ya Kiislamu kuwa eti ni kikwazo cha haki za wanawake, na kuonyesha kwamba mafundisho ya Kiislamu yamekuwa yakishikilia kanuni za haki na usawa kwa wanawake, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti.
Aidha, mkutano huo unajaribu kutayarisha mpango mpana wa mageuzi ya kisheria na kisiasa yenye lengo la kuimarisha haki na uwezeshaji wa wanawake ndani ya jamii za Kiislamu. Kiini cha mijadala hii ni upitishaji unaotarajiwa wa waraka wa kina  ambao utaelezea mipango na mikakati muhimu iliyoundwa ili kuendeleza malengo haya muhimu.
Ajenda ya mkutano inajumuisha vikao vya kazi vitano tofauti, kila kimoja kikitoa jukwaa kwa mawaziri, maafisa, wasomi, na viongozi wa fikra kuchunguza hadhi na haki za wanawake katika Uislamu.
Watatathmini kwa pamoja njia zinazowezekana za kuwawezesha wanawake wa Kiislamu katika nyanja za elimu na ajira. Zaidi ya hayo, vikao hivi vitaangazia maswala mbalimbali yanayohusiana na wanawake katika jamii za kisasa, ikionyesha dhamira ya mkutano huo kushughulikia maswala muhimu.
Mkutano wa "Wanawake katika Uislamu: Hadhi na Uwezeshaji" huko Jeddah unawakilisha juhudi kubwa ya OIC ya kukuza mazungumzo na ushirikiano juu ya mada muhimu, kwa lengo kuu la kuboresha hadhi na uwezeshaji wa wanawake ndani ya ulimwengu wa Kiislamu. Inasisitiza dhamira ya pamoja ya nchi wanachama wa OIC kukuza usawa wa kijinsia, haki, na haki za wanawake ndani ya jamii zao.

3485895

Kishikizo: wanawake waislamu oic
captcha