IQNA

Sekta ya Halal

Libya yaunda Kamati ya Kitaifa ya Bidhaa Halal

14:38 - August 23, 2022
Habari ID: 3475669
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara ya kwanza, serikali ya Libya imeanzisha kamati ya bidhaa na huduma Halal na kubainisha majukumu yake.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mohammad Al-Hawij, Waziri wa Uchumi na Biashara katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, ametoa amri ya kuanzisha kamati ya bidhaa na huduma Halal kwa lengo la kuleta taratibu na kanuni katika sekta hiyo.

Kamati iliyoundwa ina jukumu la kuunda utaratibu jumuishi wa kudhibiti huduma  na bidhaa Halal ili kuhakikisha kwamba zinafuata kanuni za Kiislamu. Aidha kamati hiyo inatazamiwa pia kuunda vigezo vya kudhibiti mchakato wa kuagiza, kufuatilia, kuangalia na kuthibitisha kuwa bidhaa au huduma husika ni Halal.

Kamati hii pia ina jukumu la kutoa mapendekezo ya mahitaji ya viwango vya kiufundi vya bidhaa za Halal, kuamua taratibu za udhibiti wa bidhaa na huduma Halal. Katika suala la nyama Halal kamati hiyo itakuwa na jukumu la  kutathmini machinjio ambayo yanaruhusiwa kutoa bidhaa zao, kuunda vigezo na utaratibu wa kuhakiki machinjio ndani na nje ya Libyam na halikadhalika kuandaawarsha za mafunzo kuhusu bidhaa na na huduma Halal.

4080158

captcha