IQNA

Sekta ya Halal

Warsha ya Kimataifa ya ‘Halal’ kufanyika Nigeria

12:16 - July 27, 2022
Habari ID: 3475548
TEHRAN (IQNA)- Warsha na maonyesho ya kimataifa kuhusu tasnia ya Halal itafanyika nchini Nigeria mwezi ujao.

Lagos, jiji kubwa zaidi barani Afrika, litakuwa mwenyeji wa hafla hiyo mnamo Agosti 8-9 na itaandaliwa na Mamlaka ya Utoaji Vyeti vya Halal ya Nigeria (HCA).

Wazungumzaji kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Mafunzo ya Halal (INHART) na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Malaysia (IIUM) watawasilisha mawazo na maoni yao kuhusu vipengele tofauti vya tasnia ya Halal.

Pia wanaozungumza katika semina hiyo watakuwa Otunba Niyi Adebayano, waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji wa Nigeria, pamoja na Muhammad Lawal Maidoki, mkuu wa Tume ya Zakat na Wakfu katika Jimbo la Sokoto.

Hotuba yake itahusu "Halal kwa Wote: Kati ya Uendelevu na Faida".

Katika semina ya mtandaoni kuhusu tasnia ya Halal ya Nigeria iliyofanyika mwaka jana kwa kushirikisha wataalam kutoka Malaysia, Pakistan, Bangladesh, na New Zealand, ilisemekana kuwa Afrika inaweza kufaidika sana na tasnia ya Halal kwa maendeleo yake ya kiuchumi.

Nigeria pia iliandaa maonyesho ya kimataifa ya Halal mnamo Septemba 2021 kwa kushirikisha makampuni kutoka Uturuki, India, Malaysia, Indonesia, Tunisia, Morocco, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Nigeria na Misri.

Neno la Kiarabu, Halal linamaanisha bidhaa au huduma ambazo zinaruhusiwa kutumika kwa sababu zimetayarishwa kwa mujibu wa Sharia (sheria za Kiislamu).

3479861

Kishikizo: halal bidhaa nigeria warsha
captcha