IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Disemba 7 ni nembo ya kupigania ukombozi dhidi ya Wamarekani

21:46 - December 07, 2022
Habari ID: 3476210
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, tarehe 16 mwezi wa Azar, (Disemba 7) ni nembo ya kupigania ukombozi na mapambano dhidi ya uistikbari.

Jumatano ya leo inasadifiana na tarehe 16 Azar kwa kalenda ya Iran ya Hijria Shamsia na ni siku ya wanachuo katika kalenda ya matukio ya Jamhuri ya Kiislamu.

Tarehe 16 Azar 1332 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 7 Disemba 1953 Miladia wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran walifanya maandamano mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran kulaani na kulalamikia ziara ya Richard Nixon, makamu wa rais wa wakati huo wa Marekani na uingiliaji wa Washington katika masuala ya ndani ya Iran. 

Maandamano hayo ya wanachuo yalikandamizwa na utawala kibaraka wa Pahlavi. Wanajeshi wa utawala huo wa kidikteta wa Shah waliua wanachuo watatu na kujeruhi mamia ya wengine kwenye maandamano ya siku hiyo. 

Mohammad Bagher Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran amesayema kwenye kikao cha leo cha wazi cha bunge kwamba, tarehe 16 Azar, ni nembo ya kupigania ukombozi, ni siku ya mapambano dhidi ya uistikbari, ni siku ya kupinga uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya Iran na ni siku ya kulaani mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Marekani nchini Iran ambayo yaliipindua serikali ya Waziri Mkuu Dk Musadiq. Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imetangaza rasmi kuhusika na mapinduzi hayo ya mwaka 1953 ya nchini Iran.

4105118

Kishikizo: bunge la Iran Qalibaf
captcha