IQNA

Spika wa Bunge la Iran katika Kongamano la Kimataifa la Wanaharakati wa Umahdi

Mapinduzi ya Kiislamu Iran yalitokana na fikra za Umahdi na Ashura

16:38 - June 07, 2022
Habari ID: 3475346
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Bunge la Iran amesema chimbuko la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni fikra za Imam Mahdi, Mwenyezi Mungu Aharikishe Kudhihiri Kwake, na Ashura.

Muhammad Baqer Qalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) ameyasema hayo leo alipohutubu katika Kongamano la Kimataifa la Wanaharakati wa Umahdi na kuongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yaliibuka katika eneo ambalo lilikuwa kitovu salama cha kuhudumia Uzayuni.

Qalibaf ameendelea kusema kuwa: "Kuhusiana na Umahdi, tunachozungumzia ni mazuri ambayo yanaashiria mustakabali mwema kwa wanadamu wote na kutimizwa matakwa yote ya Mwenyezi Mungu na Mwanadamu."

Ameongeza kuwa kuna nchi zingine duniani ambazo zinajulikana kama 'Jamhuri ya Kiislamu' lakini zinaunda muungano na maadui na hivyo maadaui hawana tabu na nchi kama hizo."

Kwingineko Qalibaf ameashiria kuhusu matatizo ya ndani ya nchi na kusema wananchi wanafahamu kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uko chini ya mashinikizo ya maadui ambao hawautakii mema mfumo huu.

Kwa msingi huo amesema Jamhuri ya Kiislamu inapaswa kudumisha nguvu na uwezo laini wake kupitia mazungumzo au kwa nguvu za kijeshi.

Spika Qalibaf amesema Marekani kamwe haiwezi kukubaliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na amesisitiza kuwa, Iran haitalegeza msimamo kuhusu muundo wa Mapinduzi ya Kiislamu.

4062538

captcha