Leo Jumapili tarehe 12 Rabiul-Awwal mwaka 1444 Hijria inayosadifiana na Oktoba 9 mwaka 2022 Miladia kwa mujibu wa moja ya riwaya, inatambulika kama siku ya kukumbuka kuzaliwa Muhammad Mustafa SAW Mtume Mtukufu wa Uislamu na hutambulika kama siku ya kuanza Wiki ya Umoja baina ya Waislamu duniani.
Waislamu wa Kisuni husherehekea tarehe 12 na wale wa Kishia tarehe 17 Rabiul -Awwal kama siku ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW
Imam Khomeini -Mwenyezi Mungu Amrehemu- Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye alikuwa mmoja wa wahubiri wa umoja duniani alitumia kipindi cha wiki hii moja ya kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul -Awwal kwa ajili ya kudumisha umoja na kukurubiana makundi mbalimbali ya Kiislamu na kukitaja kipindi hiki cha wiki moja kuwa ni Wiki ya Umoja.
Katika kikao cha leo cha wazi cha bunge, Muhammad Bageri Qalibaf Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amewapongeza Waislamu wote duniani kwa kuwadia Maulidi ya Mtume Mtukufu wa Uislamu na kuanza Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
4090445