IQNA

Sera za Kigeni za Iran

Iran yaweka vikwazo dhidi ya Umoja wa Ulaya, Uingereza kwa kuchochea ghasia, ugaidi

21:31 - December 12, 2022
Habari ID: 3476240
TEHRAN (IQNA)- Iran imewawekea vikwazo makumi ya maafisa na mashirika ya Umoja wa Ulaya (EU) na Uingereza kutokana na uungaji mkono wao na kuchochea ghasia mbaya za hivi karibuni nchini. Waliowekewa vikwazo wamekuwa wakitoa matamshi yao ya uingiliaji mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu na pia wamekuwa wakiunga mkono uungaji nchini Iran.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani, alisema, "Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kufuatia vibali kutoka kwa mamlaka husika, ndani ya mfumo wa sheria na taratibu zinazohusiana na vikwazo na katika hatua ya kulipiza kisasi, inawekea vikwazo mashirika na taasisi kadhaa za Umoja wa Ulaya na Uingereza na halikadhalika watu binafsi wa maeneo hayo kutokana na uungaji mkono wao wa makusudi kwa ugaidi na makundi ya kigaidi, na kuchochea kwao ugaidi, ghasia na chuki, ambayo imesababisha machafuko, vurugu, vitendo vya kigaidi na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya taifa la Iran."

Machafuko yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni yamekumba majimbo mbalimbali ya Iran tangu mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini alipofariki katika hospitali hiyo Septemba 16, siku tatu baada ya kuanguka katika kituo cha polisi. Uchunguzi ulihusisha kifo cha Amini na hali yake ya kiafya ya huko nyuma, na si kupigwa na polisi kama ilivyodaiwa.

Machafuko yamepelekea kupoteza maisha makumi ya raia na maafisa wa usalama, huku pia yakipelekea kuibuka mashambulio ya kigaidi kote nchini. Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, magaidi hao wanaopata himaya ya kigeni wamechoma moto mali ya umma na kuwatesa wanachama kadhaa wa Basij na vikosi vya usalama hadi kufa.

Tarehe 26 Oktoba, gaidi mwenye mafungamano na Daesh alishambulia Haram Takatifu ya Shah Cheragh katika mkoa wa kusini wa Fars kabla ya swala ya Magharibi na kuwauwa takribani waumini 15 akiwemo mwanamke na watoto wawili na kuwajeruhi wengine 40.

Takriban watu saba pia waliuawa baada ya magaidi kuwafyatulia risasi watu na vikosi vya usalama katika soko lililojaa watu katika jimbo la Khuzestan Izeh karibu na machweo ya Novemba 16.

Wizara ya Usalama ya Iran imesema Marekani na Uingereza zilichochea ghasia zilizoshuhudiwa hivi karibuni kote Iran.

Katika taarifa wiki chache zilizopita, Wizara hiyo imeongeza kuwa makumi ya magaidi wanaofungamana na utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi ya wanaopinga mapinduzi ya Kiislamu wamekamatwa katika oparesheni za kiusalama hivi karibuni.

Raia wa kigeni walionaswa wakichochea ghasia Iran wana uraia wa nchi tisa zikiwemo Ujerumani, Poland, Italia, Ufaransa, Uholanzi na Sweden.

.4106430

Kishikizo: iran ghasia machafuko
captcha