IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Waibua fujo na ghasia wamelenga uwezo wa mfumo wa Kiislamu Iran

17:57 - November 18, 2022
Habari ID: 3476109
TEHRAN(IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa leo hapa Tehran amevitaja vikosi vya usalama, jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kikosi cha jeshi la Basij kuwa nembo ya uwezo na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: kudhuru uwezo wa mfumo wa Kiislamu ni moja ya malengo ya waibua ghasia.

Akizungumza katika hotuba  kabla ya kuanza Sala ya Ijumaa leo hapa Tehran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami ameashiria ghasia na machafuko ya karibuni katika baadhi ya miji hapa nchini na kueleza kuwa:moj ya malengo makuu ya wafanya fujo hao ni kuupindua mfumo wa Kiislami na wenyewe wamekiri juu ya hilo. 

Ayatullah Khatami ameashiria hatua ya wazusha machafuko ya kuwatishia wafanya biashara kufunga masoko na maduka na kueleza kuwa: wamiliki wa maduka na wafanya biashara hawatatiliana maani vitisho hivyo vya waibua ghasia; na wale ambao waliamua kufunga maduka yao walifanya hivyo wakihofia kudhuriwa mali zao. 

Ayatullah Khatami amesema kuwa moja ya malengo ya wazusha machafuko ni kudhuru uwezo wa mfumo wa Kiislamu na kwamba serikali isiyo na uwezo haiwezi kudumisha amani na kuwadhaminia wananchi usalama. Amesema, waibua machafuko wamelenga nguvu na uwezo wa mfumo wa Kiislamu.  

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amepongeza hatua ya idara ya Mahakama ya Iran kwa kuinglia haraka suala hili na kuwafungulia mashtaka viongozi na vinara wa ghasia na machafuko ya karibuni hapa nchini na kuongeza kuwa: baadhi ya waibua machafuko wametambulika chini ya anwani tatu:  wauaji, wapinzani na wahalifu; na wanapasa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu kwa hatua zao zilizo dhidi ya usalama wa ndani, kueneza uongo, na kuvuruga mfumo wa kiuchumi, kuyumbisha usalama, na kufanya uharibifu.

4100478

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha