IQNA

Harakati za Qur'ani nchini Iran

Idadi ya waliohifadhi Qur'ani katika Majeshi ya Iran yaongezeka kwa asilimia 45

16:02 - December 26, 2022
Habari ID: 3476308
TEHRAN (IQNA) - Kamanda mwandamizi wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameesema kumekuwa na ustawi mkubwa katika kutoa mafunzo kwa wanaohifadhi Qur'ani Tukufu katika majeshi ya Iran

"Kutokana na jeshi kuhusika katika mpango wa kitaifa wa kutoa mafunzo kwa wahifadhi milioni 10 wa Qur'ani Tukufu nchini Iran, kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 45 la waliohifadhi Qur'ani Tukufu jeshini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na mpango huo unaendelea kwa mujibu wa ratiba inayofaa," Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri alisema Jumapili.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye maonyesho katika makao makuu ya Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yakionyesha mafanikio ya Qur'ani ya jeshi la Iran.

Huko nyuma mwaka 2011, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei alisema kuwa, jamii inapaswa kuchukua mwelekeo ili watu wasiopungua milioni 10 wajifunze Qur'ani Tukufu kwa moyo.

Kwingineko katika maelezo yake, Meja Jenerali Baqeri alisema kuwa vikosi vya jeshi pia vimetekeleza programu mbalimbali kwa ajili ya kukuza usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi, kuelewa, kufasiri na kutafakari kwa vikosi vyote na familia zao.

Akiashiria idadi kubwa ya makala na tasnifu kuhusu Qur'ani Tukufu katika vyuo vikuu vya Jeshi, kamanda huyo alisema mashindano mbalimbali ya Qur'ani pia yamefanyika kote nchini na kwamba mipango na matukio hayo yanapaswa kudumishwa kwa umakini katika siku zijazo.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazohusiana na ufunguzi wa maonyesho hayo.

 

3481835

captcha