IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Hamasa ya tarehe 9 Dey ilirejesha utulivu kwa taifa la Iran, njia ya Shahidi Soleimani itaendelea

21:14 - December 30, 2022
Habari ID: 3476332
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameitaja tarehe 9 Dei (30 Disemba) kuwa, muhuishaji wa dini kwa baraka za mahudhurio ya wananchi ambao walisambaratisha njama za maadui na kulirejeshea taifa hili utulivu uliokuwa umetoweka.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Kadhim Siddiquie amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kueleza kwamba, katika siku hii ya tarehe 9 Dey, kwa mara nyingine tena kulidhihirika mshikamano baina ya Imam na Umma na kuthibitisha kwamba, mafungamano baina ya Umma na Imam ambayo yalikuweko tangu mwanzoni mwa Uislamu na kuonekana mpaka leo baina ya waumini, si yenye kukatika na hakuna mtu anayeweza kuleta utengano baina ya viwili hivi.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amebainisha pia kuwa, njama za maaduii zilizofeli zililenga kutumia fitina kuzusha mfarakano baina ya Umma na Imam lakiini muono wa mbali wa wananchi ulikwamisha njama zao.

Sheikh Kazem Siddiqi ameashiria pia kuwadia hauli na mwaka wa tatu wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kueleza kuwa, shahidi Soleimani alionyesha ghera ya dini, kushikamana kikamilifu na dini na jihadi yake katika medani ya panda shuka ya mapinduzi. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesisitiza kuwa wananchi wa Iraq wataendeleza njia ya  Shahidi Soleimani hadi watakapoipigisha magoti Marekani na kuilazimu isalimu amri mbele ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tarehe 9 Dei mwaka 1388 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 30 Disemba, 2009 mamilioni ya wananchi wa Tehran na miji mingine hapa nchini walifanya maandamano kulalamikia machafuko ya barabarani na himaya ya madola ya Magharibi kwa machafuko hayo. Siku hii ya tarehe 9 Dei imepewa jina la "Siku ya Ung'amuzi na Muono wa Mbali".

4110664

captcha