IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Uwezo wa makombora wa Iran ni wa utaalamu wa ndani na uzuiaji hujuma

19:44 - November 11, 2022
Habari ID: 3476071
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, kuifanya sekta ya ulinzi ya makombora itegemee kikamilifu uwezo na utaalamu wa ndani kumeipa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nguvu za kumhofisha adui asiweze kuanzisha mashambulio.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mohammad Hassan Abu Turabi Fard, amemuelezea Shahidi Hassan Tehrani Moqaddam, Kamanda Mkuu wa kikosi cha makombora cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC kuwa ni shakhsia wa kujivunia, aliyejipambanua, kigezo na mtu wa kupigiwa mfano katika sekta ya makombora ya Iran.

Khatibu wa Sala ya Tehran, akabainisha kuwa, kuunda kombora la balestiki linalodhibitika na kuongozeka kutokea ndani na nje ya anga za juu na lenye uwezo wa kupenya kwenye mitambo yote iliyoko sasa duniani ya utunguaji makombora, bila shaka ni hatua isiyo na kifani katika kujijengea nguvu kwa kutegemea uwezo wa ndani na katika kuimarisha uwezo wa ulinzi wa kuzuia hujuma ilionao Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ametilia mkazo udharura wa kuwa macho wananchi wa matabaka mbalimbali nchini katika kukabiliana na vita vya kuchochea mifarakano vinavyoendeshwa na maadui.

Aidha amefafanua kwa kusema: "ikiwa mnaona tunao uwezo wa kudhamini usalama na harakati ya Mfumo mbele ya mtandao wa vyombo vya habari na vitamseto vinavyoendeshwa na mfumo fidhuli wa kibeberu ni kutokana na mwamko wa wananchi, wanaakademia, wanachuo, vijana na vikosi imara vinavyofanya juhudi na jitihada kubwa za kuutumikia Mfumo wa Kiislamu".

4098658

captcha