IQNA

Mashahidi wa Muqawama

Mashahidi Soleimani, Al-Muhandis walisambaratisha njama Magharibi

17:05 - January 01, 2023
Habari ID: 3476342
TEHRAN (IQNA) - Makamanda wa muqawama Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis walizuia njama za nchi za Magharibi dhidi ya Umma wa Kiislamu, kiongozi mkuu wa Kisunni wa Iraq alisema.

Rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kisunni wa Iraq Sheikh Khaled al-Mulla alisema Marekani ambayo ilishindwa kukabiliana na watu hao wawili, iliwaua katika operesheni ya kiwoga na kikunguru.

Ameyasema hayo katika hotuba yake kuelekea maadhimisho ya miaka 3 ya kuuawa kwa makamanda hao wawili.

Sheikh al-Mulla alisema maadui walikuwa wakitaka kuwasaidia magaidi kukamata Baghdad, lakini Jenerali Soleimani na al-Muhandis walisimama dhidi yao na kuharibu mpango wao.

Damu ya mashahidi hao wawili haitakuwa bure, alisema, akisisitiza haja ya kuwa macho katika vita laini ambavyo vimeilenga Iraq na makasisi.

Aliendelea kusema kuwa watu wote nchini Iraq wanapaswa kuungana ili kuijenga upya nchi hiyo.

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi  na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.

Mipango mbalimbali imepangwa kuandaliwa nchini Iran, Iraq na nchi nyingine kadhaa ili kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Jenerali Soleimani, al-Muhandi na wanajihadi wenzao.

3481894/

 

captcha