Wanazuoni na shakhsia wa kidini kutoka nchi 23 za Asia, Ulaya na Afrika wameshiriki katika mkutano huo unaojumuisha Sira ya Bibi Zahra (SA).
Kongamano hilo limeandaliwa na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) na lilifanyika siku ya Ijumaa.
Kongamano hilo lilijumuisha maonyesho ya vitabu na kazi za sanaa. Kwa mujibu wa Sheikh Ali al-Qarawi, mkurugenzi wa kamati ya wanazuoni ya mkutano huo, makala 113 za mukhtasari zimewasilishwa kwa sekretarieti ya kongamano na kwamba makala 10 bora zitakabidhiwa jopo la utafiti.
Alisema makala hizo zinahusu maisha, Sirah, khutba na mawazo ya Bibi Zahra (SA).
Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) , katika hotuba yake kwenye mkutano huo alimuelezea Hazrat Zahra (SA) kama mfano wa kina wa kuigwa na ni ruwaza njema kwa wote.
Ameongeza kuwa wanawake na wasichana wanapaswa kujifunza kuhusu tabia kamilifu ya Bibi Zahra (SA) na kumfuata kama kigezo cha kuigwa katika nyanja zote za maisha.
Sheikh Al-Karbalayi pia alibainisha kwamba mashindano ya kila mwaka ya kitabu bora, tasnifu na hadithi iliyoandikwa juu ya maisha ya Hazrat Zahra (SA) yamepangwa kufanywa idara yake
Mkutano huo wa kimataifa ulikuwa na ujumbe wa watu 12 wa wanaharakati wanawake wa Qur'ani wa Iran ambao uLItumwa Iraq na Wakfu wa Kawthar wa Shughuli za Kimataifa za Qur'ani za Wanawake.
Ujumbe huo umefanya idadi ya programu za Qur'ani katika miji ya Karbala na Najaf wakati wa kukaa kwao Iraq.
.
4115014