IQNA

Akademia ya Qur’ani Tukufu yazinduliwa Sharjah UAE

14:11 - December 27, 2020
Habari ID: 3473498
TEHRAN (IQNA) – Akademia ya Qur’ani Tukufu, ambayo imetajwa kuwa miogoni mwa kubwa zaidi duniani, imefunguliwa huko Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Akademia hiyo imefunguliwa na Sheikh Sultan bin Muhammad al Qasimi ambaye ni kiongozi mkuu wa Sharjah.

Akademia hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita mraba 75,000  na ina majumba ya makumbusho saba ya kihistoria na kisayansi.

Akizungumza katika ufunguzi huo, kiongozi mkuu wa Sharjah amesema Akademia ya Qur’ani Tukufu Sharjah ni eneo lenye harakati nyingi zenye kutoa maarifa kuhusu Qur’ani Tukufu.

3473516/

captcha