IQNA

Misahafu 40 ya kale katika Maonyesho ya Qur’ani, Sharjah UAE

19:37 - April 24, 2021
Habari ID: 3473845
TEHRAN (IQNA)- Maktaba ya umma wa Kalba katika eneo la Sharjah nchini Umoja wa Falme za Kiarabu imeandaa maonyesho ya Misahafu ya kale.

Kwa mujibu wa taarifa misahafu hiyo ni miaka 400 hadi 100 iliyopita. Mmoja ya nakala hizo za kale za Qur’ani in jina la Hassan Ridha na ina kila uziot wa kilo 10.

Maoneysho hayo yamefanyika kwa pendekezo la mwanakaligrafia maarufu wa UAE Ali Abdullah al Himadi na yanaonyesha pia historia ya kaligrafia ya Qur’ani Tukufu katika vipindi mbali mbali vya historia.

Al Himadi amekusanya misahafu ya kale kutoka nchi kama vile Jamhuri ya Azerbaijan, Uzbekistan, Romania na Kyrgyzstan. Yeye binafsi ameandaa warsha katika maonyesho hayo ambapo anatoa maelezo na umuhimu wa kaligrafia aina ya Naskh.

3474532/

captcha