IQNA

Fiqhi ya Kiislamu

Ayatullah Mobaleghi kuiwakilisha Iran katika Mkutano wa Kimataifa wa Fiqhi ya Kiislamu

13:37 - February 20, 2023
Habari ID: 3476588
TEHRAN (IQNA) – Mwanachuoni Mwandamizi wa Iran Ayatullah Ahmad Mobaleghi yuko Jeddah, Saudi Arabia, kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha 25 cha Akademia ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu.

Katika kikao hicho, atabadilishana mawazo na wanasheria washiriki kutoka nchi nyingine za ulimwengu wa Kiislamu kuhusu masuala ya ajenda ya mkusanyiko huo.

Ayatullah Mobaleghi ni mkufunzi wa kiwango cha Kharij cha Fiqh na anatambulika kama msomi wa kimataifa katika Vyuo vya Kiislamu vya Qom. Yeye pia ni mjumbe wa Baraza la Wataalamu wanamchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mkutano huo utazinduliwa mjini Jeddah leo na kuendelea hadi Februari 23. Kikao hicho kitajadili masuala na matatizo ya zama hizi na kuyazingatia kwa mtazamoa  kifiqhi na ijitihad na kubainisha hukumu zinazofaa za Shariah.

Kikao hicho pia  kinachunguza masuala kadhaa muhimu yenye mwelekeo wa kijamii na kiuchumi ambayo yanahitaji suluhisha maalum kwa mtazamo wa mafunzo ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na "kufafanua hukumu ya Shariah juu ya elimu ya lazima (ya kidini na ya kidunia) kwa wanaume na wanawake katika Uislamu", "athari za janga la Corona kwa hukumu za Shariah za ibada, familia na uhalifu", "athari za janga la Corona kwenye maamuzi ya kisheria ya mikataba, miamala, na dhima za kifedha", na "hukumu ya kuswali (Sala) kwa lugha nyingine isipokuwa Kiarabu kwa udhuru au bila udhuru na uamuzi kwa kumfuata imamu wa Sala kwa njia ya simu ya rununu au redio."

Kikao hicho pia kinajadili "kufafanua hukumu zinazohusu mitandao ya kijamii na kanuni zake", "maoni ya Shariah kuhusu watu wasiojulikana wazazi", "hukumu ya utoaji mimba kwa sababu ya ubakaji na mabadiliko ya jinsia katika Uislamu" na "jukumu la Mifumo ya Kiislamu ya ufadhili wa kijamii katika kusaidia kazi ya kibinadamu katika maeneo ya migogoro na majanga."  

Ayatollah Mobaleghi to Represent Iran at Int’l Islamic Fiqh Academy Meeting

Akademia ya Kimataifa ya Fiqh ya Kiislamu (IIFA) ni shirika la kielimu la kimataifa na ni shirika  tanzu la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, OIC. Akademia hii ilianzishwa kufuatia azimio katika Mkutano wa Tatu wa Kiislamu mnamo Januari 1981, na makao yake makuu yake Jeddah, Ufalme wa Saudi Arabia.

Wanachama wa IIFA ni wataalamu mashuhuri wa Fiqhi, wanazuoni, watafiti, na wasomi waliobobea katika nyanja za elimu za kifiqhi, kiutamaduni, kielimu, kisayansi, kiuchumi na kijamii kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu.

IIFA imepewa jukumu la kufafanua hukumu na masharti ya Shariah kuhusu masuala yanayowahusu Waislamu duniani kote, katika uhuru kamili na kwa kuzingatia Qur'ani Tukufu na Sunnah Tukufu za Mtume (SAW). Pia hufanya utafiti kuhusu masuala ya maisha ya kisasa, kufanya Ijtihad halisi na yenye ufanisi, inayolenga kutoa suluhu za Kiislamu na zilizo wazi kwa maendeleo ya fikra za Kiislamu.

4122964

Kishikizo: Fiqhi ya Kiislamu
captcha