Wakati moja alipinga hatua ya Misri ya kurejesha uhusiano wa nchi yake na utawala wa Kizayuni wa Israel na kufungwa jela kwa malalamiko yake kuhusu kadhia hiyo.
Abd al-Hamid bin Abd al-Aziz Kishk alizaliwa Machi 1933 huko Shubra Khit, mji ulioko katika Jimbo la Beheira nchini Misri. Alikwenda Maktab (shule ya Kiislamu) akiwa na umri mdogo na aliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa moyo kabla ya kumi.
Kisha akaenda katika kituo cha kidini huko Alexandria na alikuwa mwanafunzi bora katika mtihani wa mwisho wa shule za upili za Al-Azhar kote Misri. Aliingia Chuo Kikuu cha Al-Azhar na huko, pia, kulikuwa na wanafunzi wa juu.
Sheikh Kishk aliidhinishwa kuwa mwalimu katika kitivo cha misingi ya kidini cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar mwaka wa 1957. Hata hivyo, alipenda zaidi kuhubiri na ndiyo sababu aliacha ualimu katika chuo kikuu hicho.
Alitoa hotuba yake ya kwanza kwenye msikiti wa mji wake alipokuwa na umri wa miaka 12 tu. Mhubiri wa msikiti huo alichelewa kwa sababu fulani na kwa ujasiri alipanda jukwaa na kuanza hotuba ambayo aliwaalika watu wasimamie haki na watendeane wema.
Sheikh Kishk aliingia rasmi katika ulimwengu wa mahubiri mwaka 1961 na kutoa hotuba katika misikiti nchini Misri kwa miaka 20.
Mnamo 1965, alifungwa gerezani kwa ukosoaji wake wa sera za rais wa wakati huo wa Misri Gamal Abdel Nasser. Alikuwa gerezani kwa miaka 2.5 na aliteswa vikali licha ya kuwa na ulemavu wa macho. Baada ya kuachiliwa, alianza tena shughuli zake misikitini na kuanzia 1972, hotuba zake zilivutia sana nchini.
Baada ya rais wa wakati huo wa Misri Anwar Sadat kutia saini Mkataba wa Camp David, Sheikh Kishk alimkosoa Sadat na kuishutumu serikali kwa uhaini.
Sadat alitoa hotuba ya uchungu bungeni Septemba 1981 na kuwashambulia wakosoaji wake, hasa wahubiri, idadi kubwa ya wakosoaji, akiwemo Sheikh Kishk walitiwa mbaroni. Wakati huu pia, alipitia mateso makali. Baada ya Abd al-Hamid kuachiliwa kutoka gerezani mwaka wa 1982, hakuruhusiwa tena kuhubiri.